Yakobo 4:7
James 4:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia.
James 4:7 in English
James 4:7 · Berean Standard Bible
Submit yourselves, then, to God. Resist the devil, and he will flee from you.
Context
5Au mwadhani kwamba Andiko lasema bure kuwa huyo Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? 6Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Andiko husema:
“Mungu huwapinga wenye kiburi,
lakini huwapa wanyenyekevu neema.” 7Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia. 8Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili. 9Huzunikeni, ombolezeni na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.