Yakobo 3:9
James 3:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa ulimi tunamhimidi Bwana, yaani Baba yetu, na kwa huo twawalaani watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu.
James 3:9 in English
James 3:9 · Berean Standard Bible
With the tongue we bless our Lord and Father, and with it we curse men, who have been made in God’s likeness.
Context
7Kwa maana kila aina ya wanyama, ndege, wanyama watambaao na viumbe vya baharini vinafugika na vimefugwa na binadamu, 8lakini hakuna mtu awezaye kuufuga ulimi. Ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti. 9Kwa ulimi tunamhimidi Bwana, yaani Baba yetu, na kwa huo twawalaani watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu. 10Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haistahili kuwa hivyo. 11Je, chemchemi yaweza kutoa katika tundu moja maji matamu na maji ya chumvi?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.