Native Bible

James 2:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini kama mnakuwa na upendeleo kwa watu, mnatenda dhambi, na sheria inawahukumu kuwa ninyi ni wakosaji.

James 2:9 in English

James 2:9 · Berean Standard Bible

But if you show favoritism, you sin and are convicted by the law as transgressors.

Context

7Je, si wao wanaolikufuru Jina lile lililo bora sana mliloitiwa? 8Kama kweli mnaitimiza ile sheria ya kifalme inayopatikana katika Maandiko isemayo, “Mpende jirani yako kama unavyoipenda nafsi yako,” mnafanya vyema. 9Lakini kama mnakuwa na upendeleo kwa watu, mnatenda dhambi, na sheria inawahukumu kuwa ninyi ni wakosaji. 10Kwa maana mtu yeyote anayeishika sheria yote lakini akajikwaa katika kipengele kimoja tu, ana hatia ya kuivunja sheria yote. 11Kwa sababu yeye aliyesema, “Usizini,” alisema pia, “Usiue.” Basi kama huzini lakini unaua, umekuwa mvunjaji wa sheria.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.