Native Bible

James 1:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

kwa sababu mnajua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.

James 1:3 in English

James 1:3 · Berean Standard Bible

because you know that the testing of your faith develops perseverance.

Context

1Yakobo, mtumwa wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo: Kwa makabila kumi na mawili yaliyotawanyika ulimwenguni: Salamu. 2Ndugu zangu, hesabuni kuwa ni furaha tupu mnapopatwa na majaribu mbalimbali, 3kwa sababu mnajua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. 4Saburi na iwe na kazi timilifu, ili mpate kuwa wakamilifu, mmekamilishwa, bila kupungukiwa na kitu chochote. 5Kama mtu yeyote miongoni mwenu amepungukiwa na hekima na amwombe Mungu, yeye awapaye watu wote kwa ukarimu wala hana kinyongo, naye atapewa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.