Isaya 65:9
Isaiah 65:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitawaleta wazao kutoka kwa Yakobo, na kutoka kwa Yuda wale watakaomiliki milima yangu, nao watu wangu wateule watairithi, nako huko wataishi watumishi wangu.
Isaiah 65:9 in English
Isaiah 65:9 · Berean Standard Bible
And I will bring forth descendants from Jacob, and heirs from Judah; My elect will possess My mountains,* and My servants will dwell there.
Context
7dhambi zenu na dhambi za baba zenu,”
asema Bwana.
“Kwa sababu walitoa dhabihu za kuteketezwa juu ya milima
na kunichokoza mimi juu ya vilima,
nitawapimia mapajani mwao
malipo makamilifu kwa matendo yao ya zamani.” 8Hili ndilo asemalo Bwana:
“Kama vile divai mpya ingali bado inapatikana
katika kishada cha zabibu,
nao watu husema, ‘Usikiharibu,
kwa kuwa bado kuna kitu kizuri ndani yake,’
hivyo ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu;
sitawaangamiza wote. 9Nitawaleta wazao kutoka kwa Yakobo,
na kutoka kwa Yuda wale watakaomiliki milima yangu,
nao watu wangu wateule watairithi,
nako huko wataishi watumishi wangu. 10Sharoni itakuwa malisho
kwa ajili ya makundi ya kondoo,
na Bonde la Akori mahali pa kupumzikia
kwa makundi ya ngʼombe,
kwa ajili ya watu wangu wanaonitafuta. 11“Bali kwenu ninyi mnaomwacha Bwana
na kuusahau mlima wangu mtakatifu,
ninyi mnaoandaa meza kwa ajili ya Bahati,*
na kujaza mabakuli ya mvinyo uliochanganywa
kwa ajili ya Ajali,*
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.