Isaya 65:5
Isaiah 65:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
wasemao, ‘Kaa mbali; usinikaribie, kwa maana mimi ni mtakatifu mno kwako!’ Watu wa aina hiyo ni moshi katika pua zangu, ni moto uwakao mchana kutwa.
Isaiah 65:5 in English
Isaiah 65:5 · Berean Standard Bible
They say, ‘Keep to yourself; do not come near me, for I am holier than you!’ Such people are smoke in My nostrils, a fire that burns all day long.
Context
3taifa ambalo daima hunikasirisha
machoni pangu,
wakitoa dhabihu katika bustani
na kufukiza uvumba juu ya madhabahu za matofali; 4watu waketio katikati ya makaburi
na kukesha mahali pa siri,
walao nyama za nguruwe,
nazo sufuria zao zina mchuzi wa nyama zilizo najisi, 5wasemao, ‘Kaa mbali; usinikaribie,
kwa maana mimi ni mtakatifu mno kwako!’
Watu wa aina hiyo ni moshi katika pua zangu,
ni moto uwakao mchana kutwa. 6“Tazama, jambo hili hubakia limeandikwa mbele zangu:
sitanyamaza, bali nitalipiza kwa ukamilifu;
nitalipiza mapajani mwao: 7dhambi zenu na dhambi za baba zenu,”
asema Bwana.
“Kwa sababu walitoa dhabihu za kuteketezwa juu ya milima
na kunichokoza mimi juu ya vilima,
nitawapimia mapajani mwao
malipo makamilifu kwa matendo yao ya zamani.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.