Isaya 65:2
Isaiah 65:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mchana kutwa nimeinyoosha mikono yangu kwa watu wakaidi, wanaokwenda katika njia ambazo si nzuri, wafuatao mawazo yao wenyewe:
Isaiah 65:2 in English
Isaiah 65:2 · Berean Standard Bible
All day long I have held out My hands to an obstinate people * who walk in the wrong path, who follow their own imaginations,
Context
1“Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakuniulizia.
Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta.
Kwa taifa lile ambalo halikuliita Jina langu,
nilisema, ‘Niko hapa, niko hapa.’ 2Mchana kutwa nimeinyoosha mikono yangu
kwa watu wakaidi,
wanaokwenda katika njia ambazo si nzuri,
wafuatao mawazo yao wenyewe: 3taifa ambalo daima hunikasirisha
machoni pangu,
wakitoa dhabihu katika bustani
na kufukiza uvumba juu ya madhabahu za matofali; 4watu waketio katikati ya makaburi
na kukesha mahali pa siri,
walao nyama za nguruwe,
nazo sufuria zao zina mchuzi wa nyama zilizo najisi,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.