Native Bible

Isaiah 65:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: “Watumishi wangu watakula, lakini ninyi mtaona njaa; watumishi wangu watakunywa lakini ninyi mtaona kiu; watumishi wangu watafurahi, lakini ninyi mtaona haya.

Isaiah 65:13 in English

Isaiah 65:13 · Berean Standard Bible

Therefore this is what the Lord GOD says: “My servants will eat, but you will go hungry; My servants will drink, but you will go thirsty; My servants will rejoice, but you will be put to shame.

Context

11“Bali kwenu ninyi mnaomwacha Bwana na kuusahau mlima wangu mtakatifu, ninyi mnaoandaa meza kwa ajili ya Bahati,* na kujaza mabakuli ya mvinyo uliochanganywa kwa ajili ya Ajali,* 12nitawaagiza mfe kwa upanga, nanyi nyote mtainama chini ili kuchinjwa; kwa kuwa niliwaita lakini hamkuitika, nilisema lakini hamkusikiliza. Mlitenda maovu machoni pangu, nanyi mkachagua mambo yale yanayonichukiza.” 13Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: “Watumishi wangu watakula, lakini ninyi mtaona njaa; watumishi wangu watakunywa lakini ninyi mtaona kiu; watumishi wangu watafurahi, lakini ninyi mtaona haya. 14Watumishi wangu wataimba kwa furaha ya mioyo yao, lakini ninyi mtalia kutokana na uchungu wa moyoni, na kupiga yowe kwa sababu ya uchungu wa roho zenu. 15Mtaliacha jina lenu kuwa laana kwa watu wangu waliochaguliwa; Bwana Mwenyezi atawaua ninyi, lakini watumishi wake atawapa jina jingine.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.