Isaya 64:7
Isaiah 64:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hakuna yeyote anayeliitia jina lako wala anayejitahidi kukushika, kwa kuwa umetuficha uso wako na kutuacha tudhoofike kwa sababu ya dhambi zetu.
Isaiah 64:7 in English
Isaiah 64:7 · Berean Standard Bible
No one calls on Your name or strives to take hold of You. For You have hidden Your face from us and delivered us into the hand * of our iniquity.
Context
5Uliwasaidia watu wale watendao yaliyo haki kwa furaha,
wale wazikumbukao njia zako.
Lakini wakati tulipoendelea kutenda dhambi kinyume na njia zako,
ulikasirika.
Tutawezaje basi kuokolewa? 6Sisi sote tumekuwa kama mtu aliye najisi,
nayo matendo yetu yote ya uadilifu ni kama matambaa machafu;
sisi sote tunasinyaa kama jani,
na kama upepo maovu yetu hutupeperusha. 7Hakuna yeyote anayeliitia jina lako
wala anayejitahidi kukushika,
kwa kuwa umetuficha uso wako
na kutuacha tudhoofike kwa sababu ya dhambi zetu. 8Lakini, Ee Bwana, wewe ndiwe Baba yetu.
Sisi ni udongo, wewe ndiye mfinyanzi;
sisi sote tu kazi ya mkono wako. 9Ee Bwana, usikasirike kupita kiasi,
usizikumbuke dhambi zetu milele.
Ee Bwana, utuangalie, twakuomba,
kwa kuwa sisi sote tu watu wako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.