Isaya 64:3
Isaiah 64:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana ulipofanya mambo ya kutisha ambayo hatukuyatazamia, ulishuka, nayo milima ikatetemeka mbele zako.
Isaiah 64:3 in English
Isaiah 64:3 · Berean Standard Bible
When You did awesome works that we did not expect, You came down, and the mountains trembled at Your presence.
Context
1Laiti ungelipasua mbingu na kushuka chini,
ili milima ingelitetemeka mbele zako! 2Kama vile moto uteketezavyo vijiti
na kusababisha maji kuchemka,
shuka ukafanye jina lako lijulikane kwa adui zako,
na kusababisha mataifa yatetemeke mbele zako! 3Kwa maana ulipofanya mambo ya kutisha ambayo hatukuyatazamia,
ulishuka, nayo milima ikatetemeka mbele zako. 4Tangu nyakati za zamani hakuna yeyote aliyesikia,
hakuna sikio lililotambua,
hakuna jicho lililomwona Mungu mwingine ila wewe,
anayetenda mambo kwa ajili ya wale wamngojeao. 5Uliwasaidia watu wale watendao yaliyo haki kwa furaha,
wale wazikumbukao njia zako.
Lakini wakati tulipoendelea kutenda dhambi kinyume na njia zako,
ulikasirika.
Tutawezaje basi kuokolewa?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.