Isaya 63:5
Isaiah 63:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nilitazama, lakini hakuwepo yeyote wa kunisaidia, nilishangaa kwa kuwa hakuwepo yeyote aliyetoa msaada; hivyo mkono wangu wenyewe ndio ulionifanyia wokovu, na ghadhabu yangu mwenyewe ndiyo iliyonitegemeza.
Isaiah 63:5 in English
Isaiah 63:5 · Berean Standard Bible
I looked, but there was no one to help; I was appalled that no one assisted. So My arm brought Me salvation, and My own wrath upheld Me.
Context
3“Nimekanyaga shinikizo la zabibu peke yangu;
kutoka mataifa hakuna mtu aliyekuwa pamoja nami.
Nimewaponda kwa miguu katika hasira yangu
na kuwakanyaga chini katika ghadhabu yangu;
damu yao ilitia matone kwenye mavazi yangu,
na kutia madoa nguo zangu zote. 4Kwa kuwa siku ya kisasi ilikuwa moyoni mwangu,
mwaka wa ukombozi wangu umefika. 5Nilitazama, lakini hakuwepo yeyote wa kunisaidia,
nilishangaa kwa kuwa hakuwepo yeyote aliyetoa msaada;
hivyo mkono wangu wenyewe ndio ulionifanyia wokovu,
na ghadhabu yangu mwenyewe ndiyo iliyonitegemeza. 6Nilikanyaga mataifa kwa miguu katika hasira yangu,
katika ghadhabu yangu niliwalewesha,
na kumwaga damu yao juu ya ardhi.” 7Nitasimulia juu ya wema wa Bwana,
kwa matendo ambayo apaswa kusifiwa,
sawasawa na yote ambayo Bwana
ametenda kwa ajili yetu:
naam, mambo mengi mema aliyoyatenda
kwa ajili ya nyumba ya Israeli,
sawasawa na huruma zake
na wema wake mwingi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.