Isaya 62:11
Isaiah 62:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana ametoa tangazo mpaka miisho ya dunia: “Mwambie Binti Sayuni, ‘Tazama, mwokozi wako anakuja! Tazama ujira wake uko pamoja naye, na malipo yake yanafuatana naye!’ ”
Isaiah 62:11 in English
Isaiah 62:11 · Berean Standard Bible
Behold, the LORD has proclaimed to the ends of the earth, “Say to Daughter Zion: See, your Savior comes! Look, His reward is with Him, and His recompense goes before Him.”
Context
9lakini wale waivunao nafaka wataila
na kumsifu Bwana,
nao wale wakusanyao zabibu watainywa divai yake
katika nyua za patakatifu pangu.” 10Piteni, piteni katika malango!
Tengenezeni njia kwa ajili ya watu.
Jengeni, jengeni njia kuu!
Ondoeni mawe.
Inueni bendera kwa ajili ya mataifa. 11Bwana ametoa tangazo
mpaka miisho ya dunia:
“Mwambie Binti Sayuni,
‘Tazama, mwokozi wako anakuja!
Tazama ujira wake uko pamoja naye,
na malipo yake yanafuatana naye!’ ” 12Wataitwa Watu Watakatifu,
Waliokombolewa na Bwana;
nawe utaitwa Aliyetafutwa,
Mji Usioachwa Tena.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.