Isaya 61:2
Isaiah 61:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi ya Mungu wetu, kuwafariji wote waombolezao,
Isaiah 61:2 in English
Isaiah 61:2 · Berean Standard Bible
to proclaim the year of the LORD’s favor * and the day of our God’s vengeance, to comfort all who mourn,
Context
1Roho wa Bwana Mwenyezi yu juu yangu,
kwa sababu Bwana amenitia mafuta
kuwahubiria maskini habari njema.
Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo,
kuwatangazia mateka uhuru wao,
na hao waliofungwa
habari za kufunguliwa kwao; 2kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa,
na siku ya kisasi ya Mungu wetu,
kuwafariji wote waombolezao, 3na kuwapa mahitaji
wale wanaohuzunika katika Sayuni,
ili kuwapa taji ya uzuri badala ya majivu,
mafuta ya furaha badala ya maombolezo,
vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa.
Nao wataitwa mialoni ya haki,
pando la Bwana,
ili kuonyesha utukufu wake. 4Watajenga upya magofu ya zamani
na kupatengeneza mahali palipoachwa ukiwa zamani;
watafanya upya miji iliyoharibiwa,
iliyoachwa ukiwa kwa vizazi vingi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.