Isaya 60:18
Isaiah 60:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Jeuri hazitasikika tena katika nchi yako, wala maangamizi au uharibifu ndani ya mipaka yako, lakini utaita kuta zako Wokovu, na malango yako Sifa.
Isaiah 60:18 in English
Isaiah 60:18 · Berean Standard Bible
No longer will violence be heard in your land, nor ruin or destruction within your borders. But you will name your walls Salvation and your gates Praise.
Context
16Utanyonya maziwa ya mataifa,
na kunyonyeshwa matiti ya wafalme.
Ndipo utakapojua kwamba Mimi, Bwana, ni Mwokozi wako,
Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo. 17Badala ya shaba nitakuletea dhahabu,
na fedha badala ya chuma.
Badala ya mti nitakuletea shaba,
na chuma badala ya mawe.
Nitafanya amani kuwa mtawala wako,
na haki kuwa mfalme wako. 18Jeuri hazitasikika tena katika nchi yako,
wala maangamizi au uharibifu ndani ya mipaka yako,
lakini utaita kuta zako Wokovu,
na malango yako Sifa. 19Jua halitakuwa tena nuru yako mchana,
wala mwangaza wa mwezi hautakuangazia,
kwa maana Bwana atakuwa nuru yako ya milele,
naye Mungu wako atakuwa utukufu wako. 20Jua lako halitazama tena,
nao mwezi wako hautafifia tena;
Bwana atakuwa nuru yako milele,
nazo siku zako za huzuni zitakoma.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.