Isaya 59:5
Isaiah 59:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Huangua mayai ya nyoka wenye sumu kali na kutanda wavu wa buibui. Yeyote alaye mayai yao atakufa, na wakati moja lianguliwapo, nyoka hutoka humo.
Isaiah 59:5 in English
Isaiah 59:5 · Berean Standard Bible
They hatch the eggs of vipers and weave a spider’s web. Whoever eats their eggs will die; crack one open, and a viper is hatched.
Context
3Kwa maana mikono yenu imetiwa mawaa kwa damu
na vidole vyenu kwa hatia.
Midomo yenu imenena uongo,
nazo ndimi zenu zimenongʼona mambo maovu. 4Hakuna hata mmoja anayedai kwa haki;
hakuna hata mmoja anayetetea shauri lake kwa haki.
Wanategemea mabishano matupu na kusema uongo,
huchukua mimba ya magomvi na kuzaa uovu. 5Huangua mayai ya nyoka wenye sumu kali
na kutanda wavu wa buibui.
Yeyote alaye mayai yao atakufa,
na wakati moja lianguliwapo, nyoka hutoka humo. 6Utando wao wa buibui haufai kwa nguo;
hawawezi kujifunika kwa kile walichokitengeneza.
Matendo yao ni matendo maovu,
vitendo vya jeuri vipo mikononi mwao. 7Miguu yao hukimbilia kwenye dhambi,
ni myepesi kumwaga damu isiyo na hatia.
Mawazo yao ni mawazo maovu;
uharibifu na maangamizi huonekana katika njia zao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.