Isaya 59:2
Isaiah 59:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini maovu yenu yamewatenga ninyi na Mungu wenu, dhambi zenu zimewaficha ninyi uso wake, ili asisikie.
Isaiah 59:2 in English
Isaiah 59:2 · Berean Standard Bible
But your iniquities have built barriers between you and your God, and your sins have hidden His face from you, so that He does not hear.
Context
1Hakika mkono wa Bwana si mfupi hata usiweze kuokoa,
wala sikio lake si zito hata lisiweze kusikia. 2Lakini maovu yenu yamewatenga
ninyi na Mungu wenu,
dhambi zenu zimewaficha ninyi uso wake,
ili asisikie. 3Kwa maana mikono yenu imetiwa mawaa kwa damu
na vidole vyenu kwa hatia.
Midomo yenu imenena uongo,
nazo ndimi zenu zimenongʼona mambo maovu. 4Hakuna hata mmoja anayedai kwa haki;
hakuna hata mmoja anayetetea shauri lake kwa haki.
Wanategemea mabishano matupu na kusema uongo,
huchukua mimba ya magomvi na kuzaa uovu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.