Isaya 59:13
Isaiah 59:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Uasi na udanganyifu dhidi ya Bwana, kumgeuzia Mungu wetu kisogo, tukichochea udhalimu na maasi, tukinena uongo ambao mioyo yetu imeuhifadhi.
Isaiah 59:13 in English
Isaiah 59:13 · Berean Standard Bible
rebelling and denying the LORD, turning away from our God, speaking oppression and revolt, conceiving and uttering lies from the heart.
Context
11Wote tunanguruma kama dubu;
tunalia kwa maombolezo kama hua.
Tunatafuta haki, kumbe hakuna kabisa;
tunatafuta wokovu, lakini uko mbali. 12Kwa sababu makosa yetu ni mengi machoni pako,
na dhambi zetu zinashuhudia dhidi yetu.
Makosa yetu yako pamoja nasi daima,
nasi tunayatambua maovu yetu: 13Uasi na udanganyifu dhidi ya Bwana,
kumgeuzia Mungu wetu kisogo,
tukichochea udhalimu na maasi,
tukinena uongo ambao mioyo yetu imeuhifadhi. 14Hivyo uadilifu umerudishwa nyuma,
nayo haki inasimama mbali,
kweli imejikwaa njiani,
uaminifu hauwezi kuingia. 15Kweli haipatikani popote,
na yeyote aepukaye uovu huwa mawindo.
Bwana alitazama naye akachukizwa
kwamba hapakuwepo haki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.