Native Bible

Isaiah 56:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Njooni, enyi wanyama wote wa kondeni, njooni mle, ninyi wanyama wote wa mwituni!

Isaiah 56:9 in English

Isaiah 56:9 · Berean Standard Bible

Come, all you beasts of the field; eat greedily, all you beasts of the forest.

Context

7hawa nitawaleta kwenye mlima wangu mtakatifu na kuwapa furaha ndani ya nyumba yangu ya sala. Sadaka zao za kuteketeza na dhabihu zao zitakubalika juu ya madhabahu yangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.” 8Bwana Mwenyezi asema, yeye awakusanyaye Waisraeli waliohamishwa: “Bado nitawakusanya wengine kwao zaidi ya hao ambao wamekusanywa tayari.” 9Njooni, enyi wanyama wote wa kondeni, njooni mle, ninyi wanyama wote wa mwituni! 10Walinzi wa Israeli ni vipofu, wote wamepungukiwa na maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kubweka; hulala na kuota ndoto, hupenda kulala. 11Ni mbwa wenye tamaa kubwa, kamwe hawatosheki. Wao ni wachungaji waliopungukiwa na ufahamu; wote wamegeukia njia yao wenyewe, kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.