Isaya 55:1
Isaiah 55:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Njooni, ninyi nyote wenye kiu, njooni kwenye maji; nanyi ambao hamna fedha, njooni, nunueni na mle! Njooni, nunueni divai na maziwa bila fedha na bila gharama.
Isaiah 55:1 in English
Isaiah 55:1 · Berean Standard Bible
“Come, all you who are thirsty, come to the waters; and you without money, come, buy, and eat! Come, buy wine and milk without money and without cost!
Context
1“Njooni, ninyi nyote wenye kiu,
njooni kwenye maji;
nanyi ambao hamna fedha,
njooni, nunueni na mle!
Njooni, nunueni divai na maziwa
bila fedha na bila gharama. 2Kwa nini kutumia fedha kwa kitu ambacho si chakula,
na kutaabikia kitu kisichoshibisha?
Sikilizeni, nisikilizeni mimi na mle kilicho kizuri,
nazo nafsi zenu zitafurahia utajiri wa unono. 3Tegeni sikio mje kwangu,
nisikieni mimi, ili nafsi zenu zipate kuishi.
Nitafanya agano la milele nanyi,
pendo la uaminifu nililomwahidi Daudi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.