Isaya 54:16
Isaiah 54:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Tazama, ni mimi niliyemuumba mhunzi, yeye afukutaye makaa kuwa moto, na kutengeneza silaha inayofaa kwa kazi yake. Tena ni mimi niliyemwambia mharabu kufanya uharibifu mwingi.
Isaiah 54:16 in English
Isaiah 54:16 · Berean Standard Bible
Behold, I have created the craftsman who fans the coals into flame and forges a weapon fit for its task; and I have created the destroyer to wreak havoc.
Context
14Kwa haki utathibitika:
Kuonewa kutakuwa mbali nawe;
hutaogopa chochote.
Hofu itakuwa mbali nawe;
haitakukaribia wewe. 15Kama mtu yeyote akikushambulia,
haitakuwa kwa ruhusa yangu;
yeyote akushambuliaye
atajisalimisha kwako. 16“Tazama, ni mimi niliyemuumba mhunzi,
yeye afukutaye makaa kuwa moto,
na kutengeneza silaha inayofaa kwa kazi yake.
Tena ni mimi niliyemwambia mharabu
kufanya uharibifu mwingi. 17Hakuna silaha itakayofanyizwa dhidi yako
itakayofanikiwa,
nawe utauthibitisha kuwa mwongo
kila ulimi utakaokushtaki.
Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana
na hii ndiyo haki yao itokayo kwangu,”
asema Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.