Isaya 52:13
Isaiah 52:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa hekima; atatukuzwa, na kuinuliwa juu, na kukwezwa sana.
Isaiah 52:13 in English
Isaiah 52:13 · Berean Standard Bible
Behold, My Servant will prosper;* He will be raised and lifted up and highly exalted.
Context
11Ondokeni, ondokeni, tokeni huko!
Msiguse kitu chochote kilicho najisi!
Tokeni kati yake mwe safi,
ninyi mchukuao vyombo vya Bwana. 12Lakini hamtaondoka kwa haraka,
wala hamtakwenda kwa kukimbia;
kwa maana Bwana atatangulia mbele yenu,
Mungu wa Israeli atakuwa mlinzi nyuma yenu. 13Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa hekima;
atatukuzwa, na kuinuliwa juu, na kukwezwa sana. 14Kama walivyokuwa wengi
walioshangazwa naye,
kwani uso wake ulikuwa umeharibiwa sana
zaidi ya mtu yeyote
na umbo lake kuharibiwa
zaidi ya mfano wa mwanadamu: 15hivyo atayashangaza mataifa mengi,
nao wafalme watafunga vinywa vyao kwa sababu yake.
Kwa kuwa yale ambayo hawakuambiwa, watayaona,
nayo yale wasiyoyasikia, watayafahamu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.