Isaya 51:8
Isaiah 51:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana nondo atawala kama vazi, nao funza atawatafuna kama sufu. Lakini haki yangu itadumu milele, wokovu wangu kwa vizazi vyote.”
Isaiah 51:8 in English
Isaiah 51:8 · Berean Standard Bible
For the moth will devour them like a garment, and the worm will eat them like wool. But My righteousness will last forever, My salvation through all generations.”
Context
6Inueni macho yenu mbinguni,
mkaitazame dunia chini;
mbingu zitatoweka kama moshi,
dunia itachakaa kama vazi,
na wakazi wake kufa kama mainzi.
Bali wokovu wangu utadumu milele,
haki yangu haitakoma kamwe. 7“Nisikieni, ninyi mnaojua lililo sawa,
ninyi watu ambao mna sheria yangu mioyoni mwenu:
Msiogope mashutumu ya wanadamu
wala msitiwe hofu na matukano yao. 8Kwa maana nondo atawala kama vazi,
nao funza atawatafuna kama sufu.
Lakini haki yangu itadumu milele,
wokovu wangu kwa vizazi vyote.” 9Amka, Amka! Jivike nguvu,
ewe mkono wa Bwana,
Amka, kama siku zilizopita,
kama vile vizazi vya zamani.
Si ni wewe uliyemkata Rahabu vipande vipande,
uliyemchoma yule joka? 10Si ni wewe uliyekausha bahari,
maji ya kilindi kikuu,
uliyefanya barabara katika vilindi vya bahari
ili waliokombolewa wapate kuvuka?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.