Isaya 51:12
Isaiah 51:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Mimi, naam mimi, ndimi niwafarijie ninyi. Ninyi ni nani hata kuwaogopa wanadamu wanaokufa, wanadamu ambao ni majani tu,
Isaiah 51:12 in English
Isaiah 51:12 · Berean Standard Bible
“I, even I, am He who comforts you. Why should you be afraid of mortal man, of a son of man who withers like grass?
Context
10Si ni wewe uliyekausha bahari,
maji ya kilindi kikuu,
uliyefanya barabara katika vilindi vya bahari
ili waliokombolewa wapate kuvuka? 11Wale waliolipiwa fidia na Bwana watarudi.
Wataingia Sayuni wakiimba;
furaha ya milele itakuwa taji juu ya vichwa vyao.
Furaha na shangwe zitawapata,
huzuni na kulia kwa uchungu kutatoweka. 12“Mimi, naam mimi,
ndimi niwafarijie ninyi.
Ninyi ni nani hata kuwaogopa
wanadamu wanaokufa,
wanadamu ambao ni majani tu, 13kwamba mnamsahau Bwana Muumba wenu,
aliyezitanda mbingu
na kuiweka misingi ya dunia,
kwamba mnaishi katika hofu siku zote
kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu,
ambaye nia yake ni kuangamiza?
Iko wapi basi ghadhabu ya mdhalimu? 14Wafungwa waliojikunyata kwa hofu
watawekwa huru karibuni;
hawatafia kwenye gereza lao,
wala hawatakosa chakula.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.