Isaya 48:6
Isaiah 48:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Umesikia mambo haya; yaangalie hayo yote. Je, hutayakubali? “Kuanzia sasa na kuendelea nitakueleza mambo mapya, juu ya mambo yaliyofichika usiyoyajua.
Isaiah 48:6 in English
Isaiah 48:6 · Berean Standard Bible
You have heard these things; look at them all. Will you not acknowledge them? From now on I will tell you of new things, hidden things unknown to you.
Context
4Kwa kuwa nalijua jinsi ulivyokuwa mkaidi;
mishipa ya shingo yako ilikuwa chuma,
kipaji chako cha uso kilikuwa shaba. 5Kwa hiyo nilikuambia mambo haya tangu zamani,
kabla hayajatokea nilikutangazia
ili usije ukasema,
‘Sanamu zangu zilifanya hayo;
kinyago changu cha mti na mungu wangu wa chuma aliyaamuru.’ 6Umesikia mambo haya; yaangalie hayo yote.
Je, hutayakubali?
“Kuanzia sasa na kuendelea nitakueleza mambo mapya,
juu ya mambo yaliyofichika usiyoyajua. 7Yameumbwa sasa, wala si tangu zamani;
hukupata kuyasikia kabla ya siku ya leo.
Hivyo huwezi kusema,
‘Naam, niliyajua hayo.’ 8Hujayasikia wala kuyaelewa,
tangu zamani sikio lako halikufunguka.
Ninafahamu vyema jinsi ulivyo mdanganyifu,
uliitwa mwasi tangu kuzaliwa kwako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.