Isaya 48:2
Isaiah 48:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
ninyi mnaojiita raiya wa mji mtakatifu, na kumtegemea Mungu wa Israeli, Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake:
Isaiah 48:2 in English
Isaiah 48:2 · Berean Standard Bible
who indeed call yourselves after the holy city and lean on the God of Israel; the LORD of Hosts is His name.
Context
1“Sikilizeni hili, ee nyumba ya Yakobo,
ninyi mnaoitwa kwa jina la Israeli,
na mnaotoka katika ukoo wa Yuda,
ninyi mnaoapa kwa jina la Bwana,
mnaomwomba Mungu wa Israeli,
lakini si katika kweli au kwa haki; 2ninyi mnaojiita raiya wa mji mtakatifu,
na kumtegemea Mungu wa Israeli,
Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake: 3Nilitoa unabii mambo ya kwanza tangu zamani,
kinywa changu kiliyatangaza na kuyafanya yajulikane;
kisha ghafula nikayatenda, nayo yakatokea. 4Kwa kuwa nalijua jinsi ulivyokuwa mkaidi;
mishipa ya shingo yako ilikuwa chuma,
kipaji chako cha uso kilikuwa shaba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.