Isaya 45:10
Isaiah 45:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ole wake amwambiaye baba yake, ‘Umezaa nini?’ Au kumwambia mama yake, ‘Umezaa kitu gani?’
Isaiah 45:10 in English
Isaiah 45:10 · Berean Standard Bible
Woe to him who says to his father, ‘What have you begotten?’ or to his mother, ‘What have you brought forth?’”
Context
8“Enyi mbingu juu, nyesheni haki,
mawingu na yaidondoshe.
Dunia na ifunguke sana,
wokovu na uchipuke,
haki na ikue pamoja nao.
Mimi, Bwana, ndiye niliyeiumba. 9“Ole wake yeye ashindanaye na Muumba wake,
yeye ambaye ni kigae tu kati ya vigae juu ya ardhi.
Je, udongo wa kufinyangia humwambia mfinyanzi,
‘Unatengeneza nini wewe?’
Je, kazi yako husema,
‘Hana mikono’? 10Ole wake amwambiaye baba yake,
‘Umezaa nini?’
Au kumwambia mama yake,
‘Umezaa kitu gani?’ 11“Hili ndilo asemalo Bwana,
yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli na Muumba wake:
Kuhusu mambo yatakayokuja,
je, unaniuliza habari za watoto wangu,
au kunipa amri kuhusu kazi za mikono yangu? 12Mimi ndiye niliyeumba dunia
na kumuumba mwanadamu juu yake.
Mikono yangu mwenyewe ndiyo iliyozitanda mbingu,
nikayapanga majeshi yake yote ya angani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.