Isaya 44:9
Isaiah 44:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wote wachongao sanamu ni ubatili, navyo vitu wanavyovithamini havifai kitu. Wale ambao wanazitetea ni vipofu, ni wajinga, nao waaibika.
Isaiah 44:9 in English
Isaiah 44:9 · Berean Standard Bible
All makers of idols are nothing, and the things they treasure are worthless. Their witnesses fail to see or comprehend, so they are put to shame.
Context
7Ni nani basi aliye kama mimi? Yeye na atangaze.
Yeye atangaze na kuweka mbele yangu
ni kitu gani kilichotokea tangu nilipoumba watu wangu wa kale,
tena ni nini kitakachotokea:
naam, yeye na atoe unabii ni nini kitakachokuja. 8Msitetemeke, msiogope.
Je, sikutangaza hili, na kutoa unabii tangu zamani?
Ninyi ni mashahidi wangu.
Je, yuko Mungu zaidi yangu mimi?
Hasha, hakuna Mwamba mwingine;
mimi simjui mwingine.” 9Wote wachongao sanamu ni ubatili,
navyo vitu wanavyovithamini havifai kitu.
Wale ambao wanazitetea ni vipofu,
ni wajinga, nao waaibika. 10Ni nani atengenezaye mungu na kusubu sanamu,
ambayo haiwezi kumfaidia kitu chochote? 11Yeye pamoja na wenziwe wa aina yake wataaibishwa,
mafundi wao si kitu ila ni wanadamu tu.
Wote wakusanyike pamoja na kuwa na msimamo wao,
watashushwa chini kwa hofu na kwa fedheha.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.