Isaya 42:12
Isaiah 42:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wampe Bwana utukufu, na kutangaza sifa zake katika visiwa.
Isaiah 42:12 in English
Isaiah 42:12 · Berean Standard Bible
Let them give glory to the LORD and declare His praise in the islands.
Context
10Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
sifa zake toka miisho ya dunia,
ninyi mshukao chini baharini,
na vyote vilivyomo ndani yake,
enyi visiwa na wote wakaao ndani yake. 11Jangwa na miji yake na vipaze sauti zao;
makao anamoishi Kedari na yashangilie.
Watu wa Sela waimbe kwa furaha,
na wapige kelele kutoka vilele vya milima. 12Wampe Bwana utukufu,
na kutangaza sifa zake katika visiwa. 13Bwana ataenda kama mtu mwenye nguvu,
kama shujaa atachochea shauku yake,
kwa kelele ataamsha kilio cha vita,
naye atashinda adui zake. 14“Kwa muda mrefu nimenyamaza kimya,
nimekaa kimya na kujizuia.
Lakini sasa, kama mwanamke wakati wa kujifungua,
ninapiga kelele, ninatweta na kushusha pumzi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.