Isaya 38:15
Isaiah 38:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini niseme nini? Amesema nami, naye yeye mwenyewe amelitenda hili. Nitatembea kwa unyenyekevu katika miaka yangu yote kwa sababu ya haya maumivu makali ya nafsi yangu.
Isaiah 38:15 in English
Isaiah 38:15 · Berean Standard Bible
What can I say? He has spoken to me, and He Himself has done this. I will walk slowly all my years because of the anguish of my soul.
Context
13Nilingoja kwa uvumilivu hadi mapambazuko,
lakini alivunja mifupa yangu yote kama simba.
Mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu. 14Nililia kama mbayuwayu au korongo,
niliomboleza kama hua aombolezaye.
Macho yangu yalififia nilipotazama mbinguni.
Ee Bwana, ninataabika, njoo unisaidie!” 15Lakini niseme nini?
Amesema nami, naye yeye mwenyewe amelitenda hili.
Nitatembea kwa unyenyekevu
katika miaka yangu yote
kwa sababu ya haya maumivu makali
ya nafsi yangu. 16Bwana, kwa mambo kama haya watu huishi,
nayo roho yangu hupata uzima katika hayo pia.
Uliniponya
na kuniacha niishi. 17Hakika ilikuwa ya faida yangu
ndiyo maana nikapata maumivu makali.
Katika upendo wako ukaniokoa
kutoka shimo la uharibifu;
umeziweka dhambi zangu zote
nyuma yako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.