Isaya 37:31
Isaiah 37:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mara nyingine tena mabaki ya nyumba ya Yuda wataeneza mizizi chini na kuzaa matunda juu.
Isaiah 37:31 in English
Isaiah 37:31 · Berean Standard Bible
And the surviving remnant of the house of Judah will again take root below and bear fruit above.
Context
29Kwa sababu unaghadhibika na ufidhuli dhidi yangu,
na kwa sababu ufidhuli wako umefika masikioni mwangu,
nitaweka ndoana yangu puani mwako
na hatamu yangu kinywani mwako,
nami nitakufanya urudi kwa njia ile uliyoijia. 30“Hii ndiyo itakuwa ishara kwako, ee Hezekia:
“Mwaka huu utakula kile kiotacho chenyewe,
na mwaka wa pili utakula kutoka machipukizi yake.
Lakini katika mwaka wa tatu panda na uvune,
panda mashamba ya mizabibu na ule matunda yake. 31Mara nyingine tena mabaki ya nyumba ya Yuda
wataeneza mizizi chini na kuzaa matunda juu. 32Kwa kuwa kutoka Yerusalemu watakuja mabaki,
na kutoka Mlima Sayuni kundi la walionusurika.
Wivu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote,
ndio utatimiza jambo hili. 33“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana kuhusu mfalme wa Ashuru:
“Hataingia katika mji huu
wala hatapiga mshale hapa.
Hatakuja mbele yake na ngao
wala kupanga majeshi kuuzingira.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.