Isaya 35:9
Isaiah 35:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Huko hakutakuwepo na simba, wala mnyama mkali hatapita njia hiyo, wala hawatapatikana humo. Ila waliokombolewa tu ndio watakaopita huko,
Isaiah 35:9 in English
Isaiah 35:9 · Berean Standard Bible
No lion will be there, and no vicious beast will go up on it. Such will not be found there, but the redeemed will walk upon it.
Context
7Mchanga wa moto utakuwa bwawa la maji,
ardhi yenye kiu itabubujika chemchemi.
Maskani ya mbweha walikolala hapo awali
patamea majani, matete na mafunjo. 8Nako kutakuwa na njia kuu,
nayo itaitwa Njia ya Utakatifu.
Wasio safi hawatapita juu yake;
itakuwa ya wale watembeao katika Njia ile;
yeye asafiriye juu yake,
ajapokuwa mjinga, hatapotea. 9Huko hakutakuwepo na simba,
wala mnyama mkali hatapita njia hiyo,
wala hawatapatikana humo.
Ila waliokombolewa tu ndio watakaopita huko, 10waliokombolewa na Bwana watarudi.
Wataingia Sayuni wakiimba;
furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao.
Watapata furaha na shangwe;
huzuni na majonzi vitakimbia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.