Isaya 33:23
Isaiah 33:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kamba zenu za merikebu zimelegea: Mlingoti haukusimama imara, nalo tanga halikukunjuliwa. Wingi wa mateka yatagawanywa, hata yeye aliye mlemavu atachukua nyara.
Isaiah 33:23 in English
Isaiah 33:23 · Berean Standard Bible
Your ropes are slack; they cannot secure the mast or spread the sail. Then an abundance of spoils will be divided, and even the lame will carry off plunder.
Context
21Huko Bwana atakuwa Mwenye Nguvu wetu.
Patakuwa kama mahali pa mito mipana na vijito.
Hakuna jahazi lenye makasia litakalopita huko,
wala hakuna meli yenye nguvu itakayopita huko. 22Kwa kuwa Bwana ni mwamuzi wetu,
Bwana ndiye mtoa sheria wetu,
Bwana ni mfalme wetu,
yeye ndiye atakayetuokoa. 23Kamba zenu za merikebu zimelegea:
Mlingoti haukusimama imara,
nalo tanga halikukunjuliwa.
Wingi wa mateka yatagawanywa,
hata yeye aliye mlemavu atachukua nyara. 24Hakuna yeyote aishiye Sayuni atakayesema, “Mimi ni mgonjwa”;
nazo dhambi za wale waishio humo zitasamehewa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.