Isaya 31:2
Isaiah 31:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hata hivyo yeye pia ana hekima na anaweza kuleta maafa, wala hayatangui maneno yake. Yeye atainuka dhidi ya nyumba ya mwovu, dhidi ya wale ambao huwasaidia watenda mabaya.
Isaiah 31:2 in English
Isaiah 31:2 · Berean Standard Bible
Yet He too is wise and brings disaster; He does not call back His words. He will rise up against the house of the wicked and against the allies of evildoers.
Context
1Ole wao wale washukao Misri kwa ajili ya msaada,
wale wategemeao farasi,
wanaoweka tumaini katika wingi wa magari yao ya vita,
na katika nguvu nyingi za wapanda farasi,
lakini hawamwangalii yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli,
wala hawatafuti msaada kwa Bwana. 2Hata hivyo yeye pia ana hekima na anaweza kuleta maafa,
wala hayatangui maneno yake.
Yeye atainuka dhidi ya nyumba ya mwovu,
dhidi ya wale ambao huwasaidia watenda mabaya. 3Lakini Wamisri ni wanadamu, wala si Mungu,
farasi wao ni nyama, wala si roho.
Wakati Bwana atakaponyoosha Mkono wake,
yeye anayesaidia atajikwaa,
naye anayesaidiwa ataanguka,
wote wawili wataangamia pamoja. 4Hili ndilo Bwana analoniambia:
“Kama vile simba angurumavyo,
simba mkubwa juu ya mawindo yake:
hata ingawa kundi lote la wachunga mifugo
huitwa pamoja dhidi yake,
hatiwi hofu na kelele zao
wala kusumbuliwa na ghasia zao;
ndivyo Bwana Mwenye Nguvu Zote atakavyoshuka
kufanya vita juu ya Mlima Sayuni
na juu ya vilele vyake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.