Isaya 23:14
Isaiah 23:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ombolezeni, enyi meli za Tarshishi; ngome yenu imeangamizwa!
Isaiah 23:14 in English
Isaiah 23:14 · Berean Standard Bible
Wail, O ships of Tarshish, for your harbor has been destroyed!
Context
12Alisema, “Usizidi kufurahi,
ee Bikira Binti Sidoni, sasa umepondwa!
“Simama, vuka uende Kitimu;
hata huko hutapata pumziko.” 13Tazama katika nchi ya Wakaldayo,
watu hawa ambao sasa hawaonekani kama wapo!
Waashuru wameifanya nchi hiyo
kuwa mahali pa viumbe wa jangwani.
Wamesimamisha minara yao ya vita kuuzunguka,
wameziteka ngome zake na kuziacha tupu
na kuufanya kuwa magofu. 14Ombolezeni, enyi meli za Tarshishi;
ngome yenu imeangamizwa! 15Wakati huo Tiro utasahauliwa kwa miaka sabini, muda wa maisha ya mfalme. Lakini mwisho wa miaka hiyo sabini, itakuwa kwa Tiro kama ilivyo katika wimbo wa kahaba: 16“Twaa kinubi, tembea mjini kote,
ewe kahaba uliyesahauliwa;
piga kinubi vizuri, imba nyimbo nyingi,
ili upate kukumbukwa.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.