Isaya 22:4
Isaiah 22:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo nilisema, “Geukia mbali nami, niache nilie kwa uchungu. Usijaribu kunifariji juu ya maangamizi ya watu wangu.”
Isaiah 22:4 in English
Isaiah 22:4 · Berean Standard Bible
Therefore I said, “Turn away from me, let me weep bitterly! Do not try to console me over the destruction of the daughter of my people.”
Context
2Ewe mji uliojaa ghasia,
ewe mji wa makelele na sherehe!
Watu wenu waliokufa hawakuuawa kwa upanga,
wala hawakufa vitani. 3Viongozi wako wote wamekimbia pamoja,
wamekamatwa bila kutumia upinde.
Ninyi nyote mliokamatwa mlichukuliwa wafungwa pamoja,
mlikimbia wakati adui alipokuwa bado mbali. 4Kwa hiyo nilisema, “Geukia mbali nami,
niache nilie kwa uchungu.
Usijaribu kunifariji
juu ya maangamizi ya watu wangu.” 5Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, anayo siku
ya ghasia, ya kukanyaga, na ya kuogofya
katika Bonde la Maono,
siku ya kuangusha kuta
na ya kupiga kelele mpaka milimani. 6Elamu analichukua podo,
pamoja na waendesha magari ya vita na farasi.
Kiri anaifungua ngao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.