Isaya 21:8
Isaiah 21:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naye mlinzi alipaza sauti, “Mchana baada ya mchana, bwana wangu, ninasimama katika mnara wa ulinzi, kila usiku ninakaa mahali pangu nilipoamriwa.
Isaiah 21:8 in English
Isaiah 21:8 · Berean Standard Bible
Then the lookout * shouted: “Day after day, my lord, I stand on the watchtower; night after night I stay at my post.
Context
6Hili ndilo Bwana analoniambia:
“Nenda, weka mlinzi,
na atoe taarifa ya kile anachokiona. 7Anapoona magari ya vita
pamoja na kundi la farasi,
wapanda punda au wapanda ngamia,
na awe macho, awe macho kikamilifu.” 8Naye mlinzi alipaza sauti,
“Mchana baada ya mchana, bwana wangu, ninasimama katika mnara wa ulinzi,
kila usiku ninakaa mahali pangu nilipoamriwa. 9Tazama, yuaja mtu anayepanda gari la vita
pamoja na kundi la farasi.
Naye anajibu:
‘Babeli umeanguka, umeanguka!
Vinyago vyote vya miungu yake
vimelala chini vikiwa vimevunjwa!’ ” 10Ee watu wangu, mliopondwa kwenye sakafu ya kupuria,
ninawaambia kile nilichokisikia
kutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote,
kutoka kwa Mungu wa Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.