Isaya 21:13
Isaiah 21:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Neno kuhusu Arabia: Enyi misafara ya Wadedani, mnaopiga kambi katika vichaka vya Arabia,
Isaiah 21:13 in English
Isaiah 21:13 · Berean Standard Bible
This is the burden against Arabia: In the thickets of Arabia you must lodge, O caravans of Dedanites.
Context
11Neno kuhusu Duma:
Mtu fulani ananiita kutoka Seiri,
“Mlinzi, usiku utaisha lini?
Mlinzi, usiku utaisha lini?” 12Mlinzi anajibu,
“Asubuhi inakuja, lakini pia usiku.
Kama ungeliuliza, basi uliza;
bado na urudi tena.” 13Neno kuhusu Arabia:
Enyi misafara ya Wadedani,
mnaopiga kambi katika vichaka vya Arabia, 14leteni maji kwa wenye kiu,
ninyi mnaoishi Tema,
leteni chakula kwa ajili ya wakimbizi. 15Wanaukimbia upanga,
kutoka upanga uliochomolewa alani,
kutoka upinde uliopindwa,
na kutoka kwenye joto la vita.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.