Isaya 18:4
Isaiah 18:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hili ndilo Bwana aliloniambia: “Nitatulia kimya na kutazama kutoka maskani yangu, kama joto linalometameta katika mwanga wa jua, kama wingu la umande katika joto la wakati wa mavuno.”
Isaiah 18:4 in English
Isaiah 18:4 · Berean Standard Bible
For this is what the LORD has told me: “I will quietly look on from My dwelling place, like shimmering heat in the sunshine, like a cloud of dew in the heat of harvest.”
Context
2iwapelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari
kwa mashua za mafunjo juu ya maji.
Nendeni, wajumbe wepesi,
kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo,
kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu,
taifa gomvi lenye lugha ngeni,
ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito. 3Enyi mataifa yote ya ulimwengu,
ninyi mnaoishi duniani
wakati bendera itakapoinuliwa milimani,
mtaiona,
nayo tarumbeta itakapolia,
mtaisikia. 4Hili ndilo Bwana aliloniambia:
“Nitatulia kimya na kutazama
kutoka maskani yangu,
kama joto linalometameta katika mwanga wa jua,
kama wingu la umande
katika joto la wakati wa mavuno.” 5Kwa maana, kabla ya mavuno,
wakati wa kuchanua ukishapita
na maua yakawa zabibu zinazoiva,
atayakata machipukizi kwa mundu wa kupogolea matawi,
naye atakata na kuyaondoa matawi yaliyopanuka. 6Yote yataachwa kwa ajili ya ndege wawindao wa mlimani
na wanyama pori,
ndege watajilisha juu yake wakati wote wa kiangazi,
nao wanyama pori wakati wote wa masika.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.