Isaya 17:3
Isaiah 17:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mji wenye ngome utatoweka kutoka Efraimu, nao uweza wa ufalme kutoka Dameski; mabaki ya Aramu yatakuwa kama utukufu wa Waisraeli,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Isaiah 17:3 in English
Isaiah 17:3 · Berean Standard Bible
The fortress will disappear from Ephraim,* and the sovereignty from Damascus. The remnant of Aram will be like the splendor of the Israelites,” declares the LORD of Hosts.
Context
1Neno kuhusu Dameski:
“Tazama, Dameski haitakuwa tena mji
bali itakuwa lundo la magofu. 2Miji ya Aroeri itaachwa
na itaachiwa mifugo ambayo italala huko,
bila yeyote wa kuyaogopesha. 3Mji wenye ngome utatoweka kutoka Efraimu,
nao uweza wa ufalme kutoka Dameski;
mabaki ya Aramu yatakuwa
kama utukufu wa Waisraeli,”
asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 4“Katika siku ile utukufu wa Yakobo utafifia,
unono wa mwili wake utadhoofika. 5Itakuwa kama mvunaji akusanyavyo nafaka
na kuvuna nafaka kwa mikono yake,
kama wakati mtu aokotapo masazo ya masuke
katika Bonde la Warefai.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.