Isaya 16:2
Isaiah 16:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama ndege wanaopapatika waliofukuzwa kutoka kwenye kiota, ndivyo walivyo wanawake wa Moabu kwenye vivuko vya Arnoni.
Isaiah 16:2 in English
Isaiah 16:2 · Berean Standard Bible
Like fluttering birds pushed out of the nest, so are the daughters of Moab at the fords of the Arnon:
Context
1Pelekeni wana-kondoo kama ushuru
kwa mtawala wa nchi,
Kutoka Sela, kupitia jangwani,
hadi mlima wa Binti Sayuni. 2Kama ndege wanaopapatika
waliofukuzwa kutoka kwenye kiota,
ndivyo walivyo wanawake wa Moabu
kwenye vivuko vya Arnoni. 3“Tupeni shauri,
toeni uamuzi.
Wakati wa adhuhuri,
fanyeni kivuli chenu kama usiku.
Waficheni watoro,
msisaliti wakimbizi. 4Waacheni watoro wa Moabu wakae pamoja nanyi;
kuweni mahali pao pa salama ili kuepuka mharabu.”
Mtesi atafikia mwisho na maangamizi yatakoma,
aletaye vita atatoweka kutoka nchi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.