Isaya 13:14
Isaiah 13:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama swala awindwaye, kama kondoo wasio na mchungaji, kila mmoja atarudi kwa watu wake mwenyewe, kila mmoja atakimbilia nchi yake ya kuzaliwa.
Isaiah 13:14 in English
Isaiah 13:14 · Berean Standard Bible
Like a hunted gazelle, like a sheep without a shepherd, each will return to his own people, each will flee to his native land.
Context
12Nitawafanya wanadamu kuwa adimu kuliko dhahabu safi,
watakuwa wachache sana kuliko dhahabu ya Ofiri. 13Kwa hiyo nitazifanya mbingu zitetemeke,
nayo dunia itatikisika kutoka mahali pake
katika ghadhabu ya Bwana Mwenye Nguvu Zote,
katika siku ya hasira yake iwakayo. 14Kama swala awindwaye,
kama kondoo wasio na mchungaji,
kila mmoja atarudi kwa watu wake mwenyewe,
kila mmoja atakimbilia nchi yake ya kuzaliwa. 15Yeyote atakayetekwa atapasuliwa tumbo,
wote watakaokamatwa watauawa kwa upanga. 16Watoto wao wachanga watavunjwa vipande vipande
mbele ya macho yao;
nyumba zao zitatekwa
na wake zao watatendwa jeuri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.