Native Bible

Isaiah 12:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa furaha mtachota maji kutoka visima vya wokovu.

Isaiah 12:3 in English

Isaiah 12:3 · Berean Standard Bible

With joy you will draw water from the springs of salvation,

Context

1Katika siku ile utasema: “Nitakusifu wewe, Ee Bwana. Ingawa ulinikasirikia, hasira yako imegeukia mbali nawe umenifariji. 2Hakika Mungu ni wokovu wangu; nitamtumaini wala sitaogopa. Bwana, Bwana, ni nguvu zangu na wimbo wangu; amekuwa wokovu wangu.” 3Kwa furaha mtachota maji kutoka visima vya wokovu. 4Katika siku hiyo mtasema: “Mshukuruni Bwana, mliitie jina lake; julisheni miongoni mwa mataifa yale aliyoyafanya, tangazeni kuwa jina lake limetukuka. 5Mwimbieni Bwana, kwa kuwa ametenda mambo makuu, hili na lijulikane duniani kote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.