Isaya 11:5
Isaiah 11:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Haki itakuwa mkanda wake na uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake.
Isaiah 11:5 in English
Isaiah 11:5 · Berean Standard Bible
Righteousness will be the belt around His hips, and faithfulness the sash around His waist.
Context
3naye atafurahia kumcha Bwana.
Hatahukumu kwa yale ayaonayo kwa macho yake,
wala kuamua kwa yale ayasikiayo kwa masikio yake, 4bali kwa uadilifu atahukumu wahitaji,
kwa haki ataamua wanyenyekevu wa dunia.
Ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake,
kwa pumzi ya midomo yake atawaua waovu. 5Haki itakuwa mkanda wake
na uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake. 6Mbwa mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo,
naye chui atalala pamoja na mbuzi,
ndama, mwana simba na ngʼombe wa mwaka mmoja watakaa pamoja,
naye mtoto mdogo atawaongoza. 7Ngʼombe na dubu watalisha pamoja,
watoto wao watalala pamoja,
na simba atakula majani makavu kama maksai.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.