Isaya 11:15
Isaiah 11:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana atakausha ghuba ya bahari ya Misri; kwa upepo mkavu ataupeleka mkono wake juu ya Mto Frati. Ataugawanya katika vijito saba ili watu waweze kuuvuka wakiwa wamevaa viatu.
Isaiah 11:15 in English
Isaiah 11:15 · Berean Standard Bible
The LORD will devote to destruction * the gulf * of the Sea of Egypt; with a scorching wind He will sweep His hand over the Euphrates.* He will split it into seven streams for men to cross with dry sandals.
Context
13Wivu wa Efraimu utatoweka,
na adui wa Yuda watakatiliwa mbali;
Efraimu hatamwonea Yuda wivu,
wala Yuda hatakuwa na uadui na Efraimu. 14Watawashukia katika miteremko ya Wafilisti
hadi upande wa magharibi,
kwa pamoja watawateka watu nyara
hadi upande wa mashariki.
Watawapiga Edomu na Moabu,
na Waamoni watatawaliwa nao. 15Bwana atakausha
ghuba ya bahari ya Misri;
kwa upepo mkavu ataupeleka mkono wake
juu ya Mto Frati.
Ataugawanya katika vijito saba
ili watu waweze kuuvuka wakiwa wamevaa viatu. 16Itakuwepo njia kuu kwa mabaki ya watu wake
wale waliosalia kutoka Ashuru,
kama ilivyokuwa kwa Israeli
walipopanda kutoka Misri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.