Isaya 10:12
Isaiah 10:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana atakapokuwa amemaliza kazi yake yote dhidi ya Mlima Sayuni na Yerusalemu, atasema, “Nitamwadhibu mfalme wa Ashuru kwa ajili ya majivuno ya ukaidi wa moyo wake na kutazama kwa macho yenye dharau.”
Isaiah 10:12 in English
Isaiah 10:12 · Berean Standard Bible
So when the Lord has completed all His work against Mount Zion and Jerusalem, He will say, “I will punish the king of Assyria for the fruit of his arrogant heart and the proud look in his eyes.
Context
10Kama vile mkono wangu ulivyotwaa falme za sanamu,
falme ambazo vinyago vyao vilizidi vile vya Yerusalemu na Samaria: 11je, nisiishughulikie Yerusalemu na sanamu zake
kama nilivyoshughulikia Samaria na vinyago vyake?’ ” 12Bwana atakapokuwa amemaliza kazi yake yote dhidi ya Mlima Sayuni na Yerusalemu, atasema, “Nitamwadhibu mfalme wa Ashuru kwa ajili ya majivuno ya ukaidi wa moyo wake na kutazama kwa macho yenye dharau.” 13Kwa kuwa anasema:
“ ‘Kwa nguvu za mkono wangu nimefanya hili,
kwa hekima yangu, kwa sababu nina ufahamu.
Niliondoa mipaka ya mataifa,
niliteka nyara hazina zao,
kama yeye aliye shujaa
niliwatiisha wafalme wao. 14Kama mtu atiavyo mkono kwenye kiota,
ndivyo mkono wangu ulivyochukua utajiri wa mataifa;
kama watu wakusanyavyo mayai yaliyoachwa,
ndivyo nilivyokusanya nchi zote;
wala hakuna hata mmoja aliyepiga bawa
au kufungua kinywa chake kutoa mlio.’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.