Isaya 1:2
Isaiah 1:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sikieni, enyi mbingu! Sikilizeni, enyi dunia! Kwa maana Bwana amesema: “Nimewalisha watoto na kuwalea, lakini wameniasi mimi.
Isaiah 1:2 in English
Isaiah 1:2 · Berean Standard Bible
Listen, O heavens, and give ear, O earth, for the LORD has spoken: “I have raised children and brought them up, but they have rebelled against Me.
Context
1Maono kuhusu Yuda na Yerusalemu ambayo Isaya mwana wa Amozi aliyaona wakati wa utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda. 2Sikieni, enyi mbingu! Sikilizeni, enyi dunia!
Kwa maana Bwana amesema:
“Nimewalisha watoto na kuwalea,
lakini wameniasi mimi. 3Ngʼombe anamjua bwana wake,
naye punda anajua hori la mmiliki wake,
lakini Israeli hajui,
watu wangu hawaelewi.” 4Lo! Taifa lenye dhambi,
watu waliolemewa na uovu,
uzao wa watenda mabaya,
watoto waliozoelea upotovu!
Wamemwacha Bwana,
Wamemkataa kwa dharau
yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli
na kumgeuzia kisogo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.