Hosea 7:14
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hawanililii mimi kutoka mioyoni mwao, bali wanaomboleza vitandani mwao. Hukusanyika pamoja kwa ajili ya nafaka na divai mpya, lakini hugeukia mbali nami.
Hosea 7:14 in English
Hosea 7:14 · Berean Standard Bible
They do not cry out to Me from their hearts when they wail upon their beds. They slash themselves * for grain and new wine, but turn away from Me.
Context
12Wakati watakapokwenda,
nitatupa wavu wangu juu yao;
nitawavuta chini waanguke
kama ndege wa angani.
Nitakaposikia wakikusanyika pamoja,
nitawanasa. 13Ole wao, kwa sababu
wamepotoka kutoka kwangu!
Maangamizi ni yao
kwa sababu wameniasi!
Ninatamani kuwakomboa,
lakini wanasema uongo dhidi yangu. 14Hawanililii mimi kutoka mioyoni mwao,
bali wanaomboleza vitandani mwao.
Hukusanyika pamoja kwa ajili ya nafaka na divai mpya,
lakini hugeukia mbali nami. 15Niliwafundisha na kuwatia nguvu,
lakini wanapanga mabaya dhidi yangu. 16Hawamgeukii Yeye Aliye Juu Sana,
wako kama upinde wenye kasoro.
Viongozi wao wataanguka kwa upanga
kwa sababu ya maneno yao ya jeuri.
Kwa ajili ya hili watadhihakiwa
katika nchi ya Misri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.