Hosea 6:3
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tumkubali Bwana, tukaze kumkubali yeye. Kutokea kwake ni hakika kama vile kuchomoza kwa jua; atatujia kama mvua za masika, kama vile mvua za vuli ziinyweshavyo nchi.”
Hosea 6:3 in English
Hosea 6:3 · Berean Standard Bible
So let us know— let us press on to know the LORD. As surely as the sun rises, He will appear; He will come to us like the rain, like the spring showers that water the earth.
Context
1“Njooni, tumrudie Bwana.
Ameturarua vipande vipande
lakini atatuponya;
ametujeruhi lakini
atatufunga majeraha yetu. 2Baada ya siku mbili atatufufua;
katika siku ya tatu atatuinua,
ili tuweze kuishi mbele zake. 3Tumkubali Bwana,
tukaze kumkubali yeye.
Kutokea kwake ni hakika kama vile
kuchomoza kwa jua;
atatujia kama mvua za masika,
kama vile mvua za vuli
ziinyweshavyo nchi.” 4“Nifanye nini nawe, Efraimu?
Nifanye nini nawe, Yuda?
Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi,
kama umande wa alfajiri utowekao. 5Kwa hiyo ninawakata ninyi vipande vipande
kwa kutumia manabii wangu;
nimewaua ninyi kwa maneno ya kinywa changu,
hukumu zangu zinawaka
kama umeme juu yenu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.