Hosea 14:8
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ee Efraimu, nina shughuli gani tena na sanamu? Nitamjibu na kumtunza. Mimi ni kama msunobari wenye majani mabichi; kuzaa kwako matunda kunatoka kwangu.”
Hosea 14:8 in English
Hosea 14:8 · Berean Standard Bible
O Ephraim,* what have I to do anymore with idols? It is I who answer and watch over him. I am like a flourishing cypress;* your fruit comes from Me.
Context
6matawi yake yatatanda.
Fahari yake itakuwa kama mti wa mzeituni,
harufu yake nzuri kama mwerezi wa Lebanoni. 7Watu wataishi tena kwenye kivuli chake.
Atastawi kama nafaka.
Atachanua kama mzabibu,
nao umaarufu wake utakuwa
kama divai itokayo Lebanoni. 8Ee Efraimu, nina shughuli gani tena na sanamu?
Nitamjibu na kumtunza.
Mimi ni kama msunobari wenye majani mabichi;
kuzaa kwako matunda kunatoka kwangu.” 9Ni nani mwenye hekima? Atayatambua mambo haya.
Ni nani mwenye ufahamu? Huyu atayaelewa.
Njia za Bwana ni adili;
wenye haki huenda katika njia hizo,
lakini waasi watajikwaa ndani yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.