Hosea 14:4
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Nitaponya ukaidi wao na kuwapenda kwa hiari yangu, kwa kuwa hasira yangu imeondoka kwao.
Hosea 14:4 in English
Hosea 14:4 · Berean Standard Bible
I will heal their apostasy; I will freely love them, for My anger has turned away from them.
Context
2Chukueni maneno pamoja nanyi,
mkamrudie Bwana.
Mwambieni:
“Samehe dhambi zetu zote
na utupokee kwa neema,
ili tuweze kutoa matunda yetu
kama sadaka za mafahali. 3Ashuru hawezi kutuokoa,
hatutapanda farasi wa vita.
Kamwe hatutasema tena ‘Miungu yetu’
kwa kile ambacho mikono yetu wenyewe imetengeneza,
kwa kuwa kwako wewe yatima hupata huruma.” 4“Nitaponya ukaidi wao
na kuwapenda kwa hiari yangu,
kwa kuwa hasira yangu imeondoka kwao. 5Nitakuwa kama umande kwa Israeli;
atachanua kama yungiyungi.
Kama mwerezi wa Lebanoni
atashusha mizizi yake chini; 6matawi yake yatatanda.
Fahari yake itakuwa kama mti wa mzeituni,
harufu yake nzuri kama mwerezi wa Lebanoni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.